HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA YAKUSANYA MAPATO KIASI CHA BILIONI 6.4 MARA MBILI WA MWAKA JANA.Halmashauri ya mji wa KAHAMA mkoani SHINYANGA imefanikiwa kukusanya mapato kutoka vyanzo vyake vya ndani kiasi cha shilingi bilioni 6.4 ambayo ni mara mbili ya mapato ya mwaka jana yaliyokuwa shilingi bilioni 3.173.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama ANDERSON MSUMBA ambapo amesema kwa upande wa masoko halmashuri ilikuwa inakusanya milioni 20 hadi 30 lakini kwa mwaka huu wamekusanya kiasi cha shilingi milioni 144.

MSUMBA amesema kutokana na ongezeko hilo la mapato kwa sasa halmashauri inakusanya kwa mwezi kiasi cha shilingi milioni 500 ongezeko ambalo ni kubwa ukilinganisha na zamani kutokana na usimamizi mzuri waliouweka.

MSUMBA ameongeza kuwa kutokana na kuimarika kwa mapato ya ndani, halmashauri imeweza kufungua zahati 5, wodi 2 huko Kagongwa na Isagehe, walimu na watumishi wa afya kulipwa stahiki zao, pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata