ZAIDI YA VIWANJA 100 VIMEGAWIWA KIMAKOSA KATIKA ENEO LA CHUO CHA MWAMVA MJINI KAHAMA.Zaidi ya viwanja 100 zimegawiwa kimakosa kwenye eneo la chuo cha maendeleo ya wananchi Mwamva  katika halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga na kusababisha mgogoro mkubwa kwa chuo na wananchi.
 Akizungumza na wenyeviti na watendaji wa serikali za mitaa na vijiji, Mwenyekiti wa kamati ya ugawaji wa Aridhi katika Halmashauri hiyo, ANDERSON MSUMBA  ameshutumu baadhi ya viongozi hao na Maafisa wa Ardhi kwa kusababisha mgogoro huo.
Msumba amewataka viongozi hao pamoja na wananchi kutoa ushirikiano kwa Tume hiyo ili kupata ufumbuzi wa mgogoro huo wa siku nyingi.
Tume hiyo inayoongozwa na LUCAS MAKULUMO ambaye ni Diwani wa Kata ya Iyenze inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake kesho.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata