WAZIRI NGELEJA ATEMA NYONGO SAKATA LA MCHANGA WA MADINI

Dodoma. Baada ya kutajwa miongoni mwa wanaotakiwa kuchunguzwa kutokana na sakata la mchanga wa madini, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja amesema maisha hayana budi kuendelea.

Ngeleja ameyasema hayo leo Alhamisi, wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Serikali baada ya Mbunge wa Mbozi (Chadema), Paschal Haonga kuomba taarifa ya mbunge huyo wa Sengerema kutajwa kuhusika kulitia Taifa hasara kutokana na mapato ya madini.

Ingawa Mwenyekiti wa Kikao, Mussa Azzan Zungu ameikataa taarifa hiyo, lakini Ngeleja amesema:

 "Kutuhumiwa siyo kukutwa na hatia, maisha yanaendelea."

Baada ya maneno hayo machache aliendelea kutoa mchango wake.

Ngeleja na baadhi ya mawaziri wa zamani wametajwa kuhusika kwa namna moja au nyingine katika sakata la usafirishaji wa mchanga wa madini na mikataba tata ya madini nchini inayotajwa kulipotezea Taifa zaidi ya Sh100 trilioni.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata