WANAUME 15 MBARONI WILAYANI KAHAMA KWA KUWAPA MIMBA WATOTO WADOGO.



Zaidi wa watu 15 katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wamekamatwa kwa ajili kuwapa mimba watoto wadogo na Kufikishwa katika vyombo vya sheria ili kukomesha mimba za utoto wilaya humo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkuu wa wa wilaya ya Kahama FADHIL NKURLU amesema serikali imechukua hatuo hiyo kutoka na kuongeza kwa matukio hayo ya watoto kukatishwa masomoa kwa ajili ya mimba za utotoni.

NKURLU amesema watoto ni hazina na taifa la kesho ni vema kila mzazi na mlezi anawajibu wa kuhahikisha, kuwalinda na kuwalea watoto katika makuzi na madili mema ili waweze kuakisi tamaduni halisi wa mtanzania.

Katika hatua nyingine NKURLU amesema kwa wale wote wanajituchukulia sheria mkononi katika maeneo mbalimbali ya Kahama kwa kuwakata watu mapanga kwa imani za kishirikiana wametakiwa waache tabia hiyo ili wananchi wale salama na wafanyekazi za maendeleo.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata