WALIMU WA SHULE ZA MSINGI BINAFSI WILAYANI KAHAMA AMETAKIWA KUYATUMIA KIKAMILIFU MAFUNZO YA MTAALA MPYA.Walimu wa shule za msingi za binafsi wilayani Kahama mkoani shinyanga wametakiwa kuyatumia kikamilifu mafunzo ya mtaala mpya uliofanyiwa marekebisho ili kuleta mabadiliko  katika sekta ya elimu. 

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tarafa wa Tarafa ya Kahama mjini, JULIUS CHAGAMA wakati akifunga mafunzo ya mtaala mpya ulioboreshwa  yaliyofanyika katika ukumbi wa majengo  yaliyokuwa halmashauri ya Ushetu mjini Kahama. 

Amewataka washiriki kuyatumia mafunzo hayo kama chachu ya  mabadiliko na kuongeza viwango vya ufaulu katika shule wanazofundisha. 

Kwa upande wao baadhi ya walimu wameitaka serikali kuhakikisha inatoa mafunzo hayo mara kwa mara ili kuwaongezea ujuzi sawa na mabadiliko ya sekta ya elimu nchini.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata