WACHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA WAZUNGUMZIA USAJILI WA TIMU HIYO

Wachezaji wa zamani wa Simba, Zamoyoni Mogela na Selemani Motola wamezungumzia usajili wa timu hiyo mpaka hivi sasa, huku kila mmoja akieleza mtazamo wake kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano ya mimataifa.

Mogela alisema kuwa,  usajili wa Simba ni mzuri na wanaonekana watakuwa bora zaidi katika safu ya ulinzi msimu ujao, lakini haina maana ya kuwa na safu nzuri ya ulinzi halafu ushambuliaji ni butu.

"Simba wamefanya usajili mzuri mpaka wakati huu haswa nafasi ya ulinzi wameimarisha sana, ila wanachotakiwa kufanya kabla ya usajili haijafungwa ni kusajili washambuliaji wawili wa kigeni wa maana ili kuja kufunga tu, kwani kwenye ulinzi hakuna shida," alisema Mogela ambaye alishawahi kuwa mchezaji wa Yanga.

"Safu ya ulinzi ya Simba kwa usajili ulifanywa hadi sasa ni nzuri, lakini watafanya vizuri katika ligi kuu Bara, ila wakumbuke kuwa wanamichuano ya kimataifa kwa hiyo wanatakiwa kupata beki mmoja wa kati wa maana kama walivyomsajili Mwanjali basi watakuwa wamekamilisha usajili wao," alisema Matola.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata