UMESIKIA WALICHOKISEMA YANGA KUHUSU MSUVA?

Klabu ya Yanga imetoa taarifa kuwa haiwezi kumzuia mchezaji wao Saimoni Msuva endapo kuna klabu yoyote ndani na nje ya nchi itamuhitaji licha ya kuwa wao bado wanamuhitaji sana katika kikosi chao.

Taarifa hiyo ya Yanga inasema wao bado wanamkataba na mchezaji huyo mrefu na kudai wanafahamu kuna klabu nyingi zimekuwa zikimuhitaji mchezaji huyo kutokana na ubora wake na kusema wao hawana pingamizi lolote.

"Tunafahamu kuna vilabu vingi vinamtaka mchezaji wetu kutokana na ubora wake na sisi kama klabu hatuna pingamizi. Klabu yoyote ndani ya nchi na nje ya nchi inayomtaka Saimoni Msuva inakaribishwa klabuni na kufuata taratibu zote sahihi za kumnunua mchezaji. Bado Msuva ni muhimu katika klabu yetu na sisi tunapenda sana kuendelea naye lakini hatuwezi kumzuia kutafuta riziki sehemu bora zaidi kuliko kwetu" ilisema taarifa ya Yanga

Mwisho kabisa Yanga wamekanusha taarifa zinazoenea kuwa mchezaji huyo amevunja mkataba na klabu hiyo na kusema bado ni mchezaji wao.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata