TATIZO LA UKOSEFU WA MAJI LAPATIWA UFUMBUZI SHULE YA SEKONDARI DAKAMA YA USHETU KAHAMA.Tatizo la ukosefu wa maji safi na salama lililokuwa linaikabili Shule ya Sekondari ya Dakama katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga limepatiwa ufumbuzi kufuatia kukamilika kwa mradi wa maji uliojengwa katika sehemu hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu MICHAEL MATOMOLA amesema kuwa tatizo la maji limeitesa kwa muda mrefu Shule hiyo yenye vidato vya Tano na Sita hali ambayo imeweza kusababisha mgomo wa wanafunzi hivi karibuni.

Katika hatua nyingine ya maendeleo ya Halmashauri hiyo Matomora amesema ujenzi wa jengo la mpito la ofisi za Halmashauri hiyo lenye thamani ya shilingi milioni 200 umeendelea vizuri na kwamba wakati wowote wanaweza kuhamia.

Kuhusu uvumi wa maneno kwamba Halmashauri hiyo imeshindwa kujenga jengo la Ghorofa la makao makuu yake kama ilivyokuwa imepanga hapo mwazo umeshindikana; Matomora amesema mpango huo uko palepale na utekelezaji utaanza mwaka ujao wa fedha utakapoanza.

Halmashauri ya Ushetu ni moja Katika Halmashauri iliyogawika kutoka iliyokuwa Halmashauri ya wilaya ya Kahama huku ikiziacha Hamashauri ya Mji wa Kahama na Msalala nazo zikijitegema.SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata