RIPOTI MPYA KUHUSU MAUAJI YA KIBITI.

IGP Sirro
PWANI: Gazeti la UWAZI ambalo limekuwa likifuatilia matukio mbalimbali ya mauaji katika Wilaya za Kibiti, Mkuranga na Ikwiriri limeibuka na ripoti mpya ya matukio ya huko.

Waandishi wetu walioweka kambi wilayani humo walipata mapya kadhaa kwani walifanikiwa kuonana na mke wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikwiriri Kati, Kazi Bakari Mtoteke, Bi. Fatuma Athumani Mbinda ambaye ameeleza mambo ya kusikitisha katika tukio la kutekwa kwa mumewe na watu walioficha sura zao kama ninja ambapo alidai ilitokea purukushani kali kabla ya kufanikiwa kuondoka naye na mpaka sasa hajulikani alipo.

MWANAMKE ATIRIRIKA

Akizungumzia sakata hilo mwanamke huyo alikuwa na haya ya kusema: “Ilikuwa siku ya Jumatano majira ya saa mbili kasoro usiku mume wangu baada ya kumaliza kufuturu aliniaga anakwenda msikitini kuswali.

“Baada ya dakika kama tano tangu alipotoka nikasikia watu wakiongea nje ya nyumba nikajua huenda mume wangu alikuwa bado hajaenda msikitini alikuwa akiongea nao.

“Wakati nikitafakari nikashtukia mmoja amesukuma mlango na kuingia ndani ambapo wenzake wanne nao wakafuatia, nilishtuka sana nilipowaona wamevaa soksi nyeusi usoni kama maninja nikajua tumeshavamiwa na watu wabaya.

“Baada ya kuingia tu wote waliniweka chini ya ulinzi na wakaninyooshea bastola ambazo walinigusa nazo kabisa kichwani huku wakiniambia nisipowapa ushirikiano na kuwaonesha alipo mume wangu wangeniua.

“Ukweli niliona saa yangu ya kufa imefika hivyo sikuwa na jinsi zaidi ya kuwaeleza ukweli kuwa mume wangu alikuwa msikitini.

“Wakati nikiendelea kuongea nao huku nimechanganyikiwa simu yangu iliyokuwa pembeni iliingia meseji ambapo wakashtuka na mmoja wao akasema kumbe una simu eeh, hebu mpigie mumeo mwambie kuna wageni nyumbani aje haraka.
“Kwanza nilipiga namba nne,

“Kwanza nilipiga namba nne, nikawaambia simu yake haipatikani. Wakaniwekea bastola puani, kwamba watanitoa ubongo kama nafanya mchezo, ikapidi nimpigie, kweli alikuja haraka wakati huo mmoja wao alitoka nje na kujibanza sehemu fulani, mume wangu alipokuja aliingia ndani moja kwa moja ambapo ghafla walimdaka na kuanza kumpiga.

“Hapo ilitokea purukushani kwa kuwa hata yeye alijua saa yake ya kufa imefika hivyo alijaribu kutetea uhai wake lakini hata hivyo, kwa kuwa watu hao walikuwa wengi na wenye silaha walifanikiwa kumdhibiti.

“Wakati nikiangalia mume wangu anavyopambana kutetea roho yake, ukweli roho iliniuma sana na nilitamani kupiga mayowe au kulia kwa sauti lakini wengine waliniwekea bastola kichwani na kuniambia wangeanza kutoa roho yangu kama ningeendelea kupiga kelele.

“Waliniambia nilale kifudifudi nisiangalie wanachomfanyia mume wangu ambapo walitumia muda huo kuondoka naye.

“Baada ya kuondoka naye nilipopata mwanya nilikimbilia Kituo cha Polisi cha Ikwiriri kutoa taarifa hiyo ambapo walifungua jalada la uchunguzi wa tukio hilo na kuniahidi kumtafuta mume wangu.

“Mpaka sasa sijui kama mume wangu yuko hai au amekufa lakini namuombea Mungu mume wangu awe hai maana ameniachia mzigo wa watoto wanne wanaohitaji kuendelezwa kimasomo na mimi sina uwezo wa kuwalea peke yangu.

“Namuomba IGP Simon Sirro kupitia jeshi la polisi anisaidie kufanikisha kupatikana kwa mume wangu akiwa hai.”

Wakati mwenyekiti huyo akitekwa, Juni 9 watu watatu walipigwa risasi na kuchukuliwa na watu waliowapiga risasi katika Kijiji cha Nyamisati, Kibiti Rufiji na kupelekwa kusikojulikana kwa mujibu wa wanavijiji wa Nyamisati.

MKE MWINGINE ASIMULIA
Aisha Omari, mke wa Hamisi Mtambo, mmoja wa majeruhi wa risasi na aliyechukuliwa na waliofanya kitendo hicho, alisema watu hao walivunja mlango wa nyumba yao na kumuua mumewe kwa kumchoma visu na kumpiga risasi.

“Walitoka nje wakaingia baadaye na kuuchukua mwili wa mume wangu kwa kuuburuza kisha wakaupakia kwenye gari… walitaka niwaonyeshe silaha alizokuwa anatumia mume wangu, nikawaambia sijawahi kuona akitumia silaha kwa kuwa yeye ni mgambo tu,” alisema.

Alidai hata mtoto wake wa miaka mitatu na nusu alipigwa ili aseme ukweli naye akasema hajawahi kuona silaha, wakaondoka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga alithibitisha kutokea kwa tukio la kutekwa Mtoteke na akasema polisi wameshafungua jalada la uchunguzi kufuatia tukio hilo.
Aidha, tukio la kupigwa risasi kwa Mtambo na wenzake Kamanda Lyanga alisema amepata taarifa kwamba wananchi wanadai waliona miili ya watu hao ikichukuliwa na hao waliofanya uhalifu huo na kuipakia katika gari nyeupe aina ya Land Rover.
“Mpaka sasa hatujajua wahalifu hao wameipeleka wapi miili hiyo, hivyo tunafanya uchunguzi ili kubaini mahali walipoipeleka, mmoja alikuwa mwanaume na mwingine mwanamke,” alisema Kamanda Lyanga.
Wakati huo huo, Mgambo wa Kijiji cha Ikwiriri aliyepigwa risasi ya kichwa akiwa shambani akivuna ufuta, Nurdini Kisinga aliyelazwa Hospitali ya Mchukwi iliyopo Kijiji cha Songa Ikwiriri hali yake imeelezwa kuwa nzuri na kuruhusiwa kutoka hospitali.

AKIMBIA NYUMBA
Ijumaa iliyopita wanahabari wetu walikwenda hospitalini hapo na kukutana na mmoja wa maofisa wa hospitali hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Rajabu Kaimu ambaye alithibitisha majeruhi huyo kulazwa hospitalini hapo na kuruhusiwa baada ya kupata nafuu.

“Ni kweli huyo mgonjwa tulikuwa naye hapa, alitibiwa na kupewa rufaa ya kwenda kutibiwa zaidi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili lakini alitokea daktari mwingine ambaye alisema atamtibia hapahapa.

Na kweli alimtibia mpaka akapata nafuu kabisa ambapo jana ameruhusiwa kurudi nyumbani,” alisema Kaimu.

Wanahabari walielekezwa nyumbani kwa majeruhi na mmoja wa wakazi wa Ikwiriri ambapo walifika kwenye nyumba hiyo na walikuta kufuli kubwa likining’inia.

Kutokana na nyumba hiyo kuwa peke yake walikosa majirani wa kuwauliza alipo majeruhi huyo hata hivyo, wanahabari wetu walitembea mita kama mia na kukuta nyumba zingine ambazo nazo zinaning’inia makufuli ikielezwa nao wamezikimbia kufuatia hofu ya wauaji hao.

Hata hivyo, walizidi kuwatafuta majirani ambao wengi walikuwa wakikimbia baada ya wanahabari wetu kusimamisha gari karibu yao na kushuka.

Baadaye walimpata jirani mmoja ambaye alisema majeruhi huyo ameamua kwenda kuishi mafichoni kuhofia watu hao walioonekana kudhamiria kumtoa roho yake maana ni Mungu tu amesalimika.

WAZIRI NA IGP
Wakati Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akisema matukio ya mauaji ya hivi karibuni mkoani Rufiji yana harufu ya kisiasa, Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP), Simon Sirro (pichani) amevitaka vyombo vya habari kuwa na uzalendo, ikiwa ni pamoja na kuacha kutoa taarifa zenye kuchochea hofu kwa wananchi.

Waliyasema hayo kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki iliyopita katika Mikoa ya Singida na Morogoro. Waziri Mwigulu Akihutubia wananchi katika Kijiji cha Kaselya wilayani Iramba, Singida alisema anahusisha mauaji hayo na siasa kwa kuwa mauaji ya wananchi kwenye maeneo hayo yanawakumba zaidi wafuasi na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alihoji: “Ujambazi gani huo wa Wana CCM tu? Hako kamchezo tumeshakagundua. Dhahiri, huo ni ushamba wa vyama vingi.”

Aliongeza kuwa, wanaodhani kuwa upinzani ni kwenye maisha wanakosea na siasa hazipaswi kuwa za uadui.

Naye IGP Sirro amevitaka vyombo vya habari nchini kuwa na uzalendo ikiwa ni pamoja na kuacha kutoa taarifa zenye kuchochea hofu kwa wananchi.

Kuhusu mauaji yanayotokea katika Wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani, alisema vyombo vya dola vinaendelea kuyadhibiti kwa kuchukua hatua.

“Taarifa zinazotolewa kwa umma hazioneshi kama kuna kazi inafanyika na vyombo vya dola kuzima mauaji hayo,” alisema.

IGP Sirro aliwataka wanahabari wanapoandika masuala ya kiusalama, watafute ufafanuzi kwenye vyombo husika ili waandike taarifa sahihi, ikiwa ni pamoja na kutanguliza uzalendo mbele huku wakitambua athari zinazotokana na taarifa hizo kwa jamii.

Source: Global Publisher

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata