RAIA WAANDAMANA KUPINGA MAREKEBISHO YA KATIBA MALI

Maelfu ya raia yaandamana mjini Bamako kupinga marekebisho ya katiba nchini Mali

Muungano wa A BANNA ulitoa wito wa maandamano kupinga mpango wa kura ya maomi yenye lengo la kufanyia marekebisho katiba nchini Mali.

Serikali ya Bamako ilipanga kuendesha kura ya maomi kwa lengo la kubadilisha katiba.

Zoezi la kura hiyo ya maoni inatarajiwa kufanyika ifikapo Julai 9 mwaka 2017.

Katika maandamano hayo raia wameitaka serikali kutoifanyia marekebisho katiba.

Zaidi ya watu 300 000 waliandamana kupinga mpango huo wa serikali ya Bamako wa kubadilisha katiba.

Ni mara ya pili kufanyika maandamano ya kupinga marekebisho ya katiba ambapo maandamano ya kwanza waandamanaji walitawanywa na Polisi.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata