PAPA FRANCIS AWAPIGA MKWARA MAPADRI NIGERIA

Rome. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, amelitaka kundi la mapadri nchini Nigeria waahidi kumtii na kuheshimu uamuzi wake la sivyo wafukuzwe kutoka kwenye kanisa hilo.

Amesema hayo kutokana na hatua ya makasisi katika Jimbo la Ahiara kumkataa askofu aliyeteuliwa mwaka 2012.

Papa aliwaambia waumini wa kanisa hilo kutoka Nigeria waliokuwa Roma wiki iliyopita kwamba ‘watu wa Mungu wameshangazwa sana’ na yaliyotokea.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya kidini, Martin Bashir amesema ni nadra sana kwa Papa kutoa vitisho vya aina hiyo.

Amewapa makasisi hao hadi tarehe 9 Julai waandike barua wakiahidi kumtii na waombe msamaha.

Rais wa Chama cha Maaskofu wa Nigeria, Askofu Mkuu, Ignatius Kaigama, alikuwa katika mkutano huo mjini Roma na aliiambia BBC kwamba Papa Francis amesikitishwa sana na yaliyokuwa yakitokea na kwamba ungeona "uchungu kwenye macho yake."

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata