MUUZA NDIZI WA MIAKA 94 ALIYEPORWA INDONESIA ACHANGIWA PESA

Watu nchini Indonesia wameungana kumsaidia mzee mmoja muuza ndizi ambaye anasema kuwa aliiporwa zaidi ya rupiah milioni 1 au dola 80.

Suratman mwenye umri wa miaka 94, aliombwa na dereva mmoja aingie kwenye gari lake ili auze matunda.


Akiwa ndani ya gari hilo wanaume hao walimlazimisha Bwana Suratman kutoa pesa zote kwa mfuko, kisha wakamtupa nje na kutoroka kwa gari lao.

Tommy Reza alichapisha video ya Bwana Suratman akiwa mwenye mawazo ambayo imevutia huruma na watu kutoa mchango.


Kisa hicho kilitokea mkoa wa Jambi katika kisiwa cha Sumtara. Tommy Reza aliambia BBC kuwa alimpata Bwana Suratman akiwa mwenye majonzi.

"Nilikuwa eneo hilo wakati nilimuona mwanamume akipiga kelele akiomba msaada," alisema Reza.

 Tangua video hiyo iweke kwenye mitandao ya zaidi ya rupiah milioni 37, zaidi ya dola 2900 zimechangwa.
Gavana wa eneo hilo baadaye alitoa rupiah milioni 5. Kisha bwana Reza akachapisha picha akimkabidhi Suratman pesa hizo.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata