MAONESHO YA 41 YA SABASABA MWAKA HUU KUANZA JUNI 28

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tantrade) , Theresia Chilambo akizungumza na waandishi habari juu ya maonesho ya 41 yatayoanza Juni 28 katika viwanja vya Sabasaba leo jijini Dar es Salaam.
Watanzania wameaswa kujitokeza katika maonesho ya 41 ya Biashara ya kimatifa jijini Dar es salaam yanayotarajia kuaanza June 28 mwaka huu katika kuangalia fursa mbalimbali za kibiashara zinazotokana na sekta ya Kilimo ilikuweza kufikia uchumi wakati unaolenga maendeleo ya viwanda.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tantrade) , Theresa Chilambo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi yanayoendelea katika Viwanja Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa maaonesho ya mwaka huu yanatarajiwa kuwa nafursa nyingi za kilimo biashara kutokana makapuni mengi ya kimataifa kutaka kushiriki na kukuza ushiriki wao ilikuweza kutoa hamasa kwa mkampuni ya ndani.
‘’Mwaka huu kutakwa na banda maalum litakalohamasisha watanzania na wadau wa nje ya nchi kuweza kuhamasika kuweza kununua bidhaa za ndani ilikuhamasisha mchakato mzima wa made in Tanzania’’amesema Thesia chilambo.
Sehemu ya mafundi wakiwa katika ukarabati katika mabanda mbalimbali katika vwanja vya sabasaba.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata