MABAHARIA 7 WAPATIKANA WAMEFARIKI KATIKA AJALI YA MELI YA JESHI LA MAREKANI

Mabaharia saba wamepatikana wakiwa wamefariki dunia baada ya meli ya jeshi la Marekani ilipogongana na meli ya mizigo ambayo ilikuwa na bendera ya Ufilipino katika maeneo ya bahari ya Japan.

Maiti hizo zilipatikana ndani ya meli katika chumba cha kulala ambacho kiliharibika na kujaa maji.

Meli ya mizigo ilikuwa ni aina ya ACX Crystal iliyokuwa na urefu wa mita 222 na meli ya kijeshi ya Marekani ina urefu wa mita 154 ambayo pia huwa inatumika katika kuharibu makombora.

Mmoja kati ya makamanda wa jeshi la Marekani alijeruhiwa katika ajali hiyo na alikimbizwa haraka hospitalini usafiri wa helikopta.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata