BODA BODA KAHAMA WACHOMA MASHAMBA BAADA YA KUKUTA MIILI YA WENZAO WALIOUWAWA KATIKA MASHAMBA HAYO.KAHAMA
Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni madereva bodaboda wa mjini Kahama wamekutwa wakiwa wamekufa katika Shamba la miti linalomilikiwa na mkulima, MARKO NKULI katika eneo la Nyakato wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Watu hao ambao majina yao hayakufahamika mara moja, wamekutwa katika eneo hilo kufuatia msako uliofanywa na madereva bodaboda katika mashamba hayo wakimtafuta dereva mwenzao aliyekuwa amepotea na kukutwa ameuawa kwenye msitu huo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Baadhi ya madereva Bodaboda wameiambia Kijukuu Blog kuwa miili hiyo imekutwa ikiwa na majereha sehemu mbali mbali huku viungo vingine vya binadamu likiwemo fuvu la kichwa eneo vikiwa katika eneo hilo.

Wakiongea mbele ya ofisi ya mkuu wa  wilaya, Madereva hao wameiomba serikali kumnyang’anya mmiliki huyo eneo hilo kwani limekuwa likitumika kama kichaka cha kujifichia wahalifu wanaowateka na kuwauwa madereva bodaboda na kuchukua pikipiki zao.

Katika hatua nyingine madereva hao wamevamia na kuchoma moto mashamba hayo ya miti yanayokadiriwa kuwa na ukubwa wa heka 50 huku wakisema kuwa uamuzi huo umelenga kusafisha eneo hilo ambalo linadaiwa kuficha wahalifu.

Nao baadhi ya majirani wanaoishi kuzunguka mashamba hayo wamepongeza uamuzi huo wa madereva boda boda kuchoma eneo hilo, na kuongeza kuwa wamekuwa wakiishi kwa hofu kutokana na uwepo wa vichaka hivyo.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha upelelezi Polisi Kahama, GEORGE BAGEMU amesema kuwa watuhumiwa watatu wa mauaji hayo wamekamatwa Kakonko mkoani Kigoma na watasafirishwa kuletwa Kahama kwa ajili ya hatua zaidi za upelelezi.

Tukio hilo linajiri wakati ambapo kumekuwa na ongezeko la matukio ya kutekwa kwa madereva bodaboda na pikipiki zao kuibiwa wilayani Kahama.

MATUKIO KATIKA PICHA:
 ENEO LA MASHAMBA YA MWANA NKULI NYAKATO LIKITEKETEA KWA MOTO BAADA YA MADEREVA BODA BODA KULICHOMA.

 MAAFISA WA POLISI WAKISHUSHA MIILI YA MADEREVA BODA BODA NA FUVU LA KICHWA ILI KUHIFADHIWA KATIKA CHUMBA CHA MAITI KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA.

 MADEREVA BODA BODA WAKIWA KATIKA OFISI YA MKUU WA WILAYA WAKIHITAJI KUONGEA NA MKUU WA WILAYA KUHUSU ENEO LA MSITU WA MWANANKULI.

 HUDUMA ZA USAFIRI WA BODA BODA LEO ZILISIMAMA KWA MUDA BAADA YA MADEREVA BODA BODA KUANDAMANA WAKIHITAJI KUONGEA NA MKUU WA WILAYA.
 AFISA WA POLISI AKIWASIHI MADEREVA BODA BODA WALIOKUWA NJE YA GETI LA MOCHWARI KUTULIA WAKATI SWALA LAO LIKIFANYIWA KAZI.

 MASHAMBA YA MZEE NKULI YAKIENDELEA KUTEKETEA BAADA YA KUCHOMWA MOTO.
 ENEO LA MWANANKULI BAADA YA KUCHOMWA MOTO.
 MOTO UKIZIDI KUSAMBAA MAENEO MBALI MBALI YA MASHAMBA YA MWANA NKULI.

 MIILI YA BODA BODA ILIYOKUTWA KATIKA MSITU WA MWANANKULI IKIINGIZWA MOCHWARI.

 ASKARI WA KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI WAKIUZIMA MOTO ULIOKUWA UNAELEKEA KATIKA SHULE YA SUNSET.

 MAAFISA POLISI WAKIENDELEA KUSHUSHA MIILI YA MADEREVA BODA BODA.
 MADEREVA BODA BODA WAKIWA NJE YA GETI KUU LA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA.
 SHULE YA MSINGI SUN SET AMBAYO IKO KARIBU NA MSITU HUO,AMBAPO MOTO ULIKWA UMEAANZA KUIFIKIA.

 GARI LA ZIMA MOTO TOKA BUZWAGI LIKITOA MSAADA WA KUZIMA MOTO KATIKA ENEO LA SHULE YA SUNSET.
 ASKARI WA KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI WAKIENDELEA KUZIMA MOTO.
SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata