KAGO SACCOS YA KAHAMA WAPINGA UAMUZI WA SERIKALI KUPIGA MNADA MALI ZAKE.Chama cha ushirika cha Kago Saccos cha mjini Kahama kimepinga uamuzi wa serikali mkoani Shinyanga wa kuuza mali zake baada ya mkutano mkuu uliofanyika Ijumaa iliyopita kupitisha maazimio ya kuuza baada ya kushindwa kumudi gharama za maisha na uendeshaji wa ofisi za ushirika huo zilizoko kata ya Malunga.

Mwenyekiti wa Saccos hiyo Emmanuel Sylvester amesema serikali haiwezi kuzuia ushirika huo kuuza mali zake kwa kuwa haina mchango wowote iliyochangia kuanzishwa kwake ambao wameamua kuuza baada ya kufilisika kutokana na serikali hiyo hiyo kuwazuia kubeba mizigo mashineni.

Sylvester amesema ushirika huo ulianzishwa mwaka 2003 na 2014 ulitokea mgogoro kati yake na wamiliki wa mashine hali iliyopelekea serikali kuwazuia kubeba mizigo wakati wao walisajiriwa kwa ajili ya shughuli hiyo na baada ya kusimama hali ya maisha ilizidi kuwa ngumu ndipo Juzi Ijumaa walikaa mkutano mkuu na kuamua kuuza kwa mali zake.

Hata hivyo katibu tawala msaidizi wa mkoa wa Shinyanga Mohamed Nchira amesema wao kama serikali hawana kipingamizi cha kuuza mali zao isipokuwa wamezuia baada ya kuona taratibu za uuzaji zimekiukwa ikiwa ni pamoja na kufanya mkutano mkuu wakati tayari walishatangaza kuuza kinyume cha taratibu.

Nchira amesema Saccos yao wanapaswa kuuza kwa kufuata sheria na taratibu na kuongeza kuwa Juzi wamekaa nao na kuwapa ushauri lakini baada ya siku moja ya mkutano mkuu walianza kuuza mali wakati wanapaswa kutanguliwa kwa mkutano mkuu na ndipo kuweka matangazo ya mnada kwa kibali cha mrajisi wa vyama vya ushirika hali ambayo hawakufanya.

 Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo amesema Saccos hiyo ilianza na wanachama 25 na sasa wapo 23 baada ya wenzao wawili kufariki hali ambayo polisi wakiongozwa na mkuu wa upelelezi wa wilaya ya Kahama George Baghem leo asubuhi wakiwa kwenye magari mawili yaliyojaa polisi walitanda katika ofisi hizo zilizopo kata ya Malunga kuzuia mnada huo ambao ulikuwa umetangazwa kufanyika leo saa 4 asubuhi.SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata