JUMA NYOSSO ATINGA KAGERA SUGAR, ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI


HATIMAYE beki mahiri wa zamani wa Ashanti, Simba na Mbeya City, Juma Said Nyosso amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Kagera Sugar.

Nyosso ambaye amemaliza adhabu yake ya kufungiwa kucheza soka kwa miaka miwili na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baada ya kumdhalilisha aliyekuwa mshambuliaji wa Azam, John Bocco alisaini mkataba huo jana.

Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, beki huyo ambaye alikuwa akifanya mazoezi kwa kipindi chote ambacho alikuwa nje ya ligi alikubali kujiunga na Kagera badala ya timu kadhaa zilikuwa zinatajwa kumwania ikiwemo Simba.

“Nyosso amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Kagera na tunaamini kuwa atafanya vizuri sana kwa kuwa wachezaji wengi waliowahi kuitumikia timu hii alishawahi kuwa nao kwenye klabu moja akiwemo Juma Kaseja,” kilisema chanzo hicho.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata