HUYU NDIYE MCHEZAJI MPYA WA SIMBA

Asubuhi ya leo Juni 15, 2017 zilitoka taarifa kwamba, klabu ya Simba imesainisha Ally Shomari mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba, taarifa ambazo pia ziliripotiwa na mtandao huu (www.shaffihdauda.co.tz).

Kiungo huyo kiraka kutoka klabu ya Mtibwa Sugar, ametambulishwa rasmi na makamu wa Rais wa Simba Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ kwa kukabidhiwa jezi ya klabu hiyo.

Ally Shomari anakuwa mchezaji wa saba kusaini mkataba kuitumikia Simba akiwa ametanguliwa na John Bocco, Shomari Kapombe, Aishi Manula, Jamal Mwambeleko, Benedict Haule na Yusuph Mlipili.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata