DEREVA NA KONDA WA BASI LA OSAKA RAHA MBARONI KWA KUSAFIRISHA BANGI.

Msako mkali unaoendesha na Jeshi la polisi mkoani Tabora umefanikisha kuwatia mbaroni watumishi wawili wa basi la kampuni ya Osaka Raha inayofanya safari zake kutoka mkoani Kagera kwenda jijini Dar es salaam wakiwa na mifuko mitatu ya bangi wakiwa wanaisafirisha kinyume cha sheria,wakiwa wameficha harufu yake kwa vitunguu vilivyosagwa.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani Tabora Kamanda wa polisi mkoani humo Kamishna Msaidizi Mwandamizi Millibroad Mtafungwa amewataja majina kuwa ni William Michael (34)dreva,mkazi wa Dar es salaam,na Leonard Astoni (42) Kondacta naye wa Dar es salaam,watumishi wa basi hilo la Osaka Raha,lenye namba za usajili T968CPC.

Aidha amesema kuwa,msako huo umefanikisha kumkamata mtu mmoja Bw,Yasini Salum (580) mkazi wa Sikonge akiwa na vipande 5 vya meno ya tembo vikiwa na thamani ya zaidi shilingi milioni 33,ambapo upelelezi unaendelea ili ijulikane alikuwa anayapeleka wapi na baadae atafikishwa mahakamani.

Kutokana na kufanikisha kukamatwa kwa vitu hivyo amewataka wananchi wa mkoani Tabora kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuokoa vijana na bangi pamoja na rasilimali za nchi.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata