BODA BODA KAHAMA WAKAMATA PIKIPIKI SITA ZINAZODHANIWA KUTUMIKA KATIKA VIDENDO VYA UHALIFU.Umoja wa daladala za pikipiki wilayani KAHAMA (UDAPI), umefanikiwa kukamata pikipiki sita zinazodhaniwa kutumika katika vitendo vya uhalifu katika maeneo mbali mbali wilayani humo.

Akizungumza Kijukuu Blog, Mwenyekiti wa UDAPI, IDSAM MAPANDE amesema pikipiki hizo wamezikamata kwenye operesheni maalum ya kuhakiki pikipiki zinazotoa huduma ya usafiri wa abiria ili kujua kama zimesajiliwa kihalali.

MAPANDE amesema operesheni hiyo ambayo inafanyika kwa ushirikiano na vyombo vya dola, inatokana na matukio ya hivi karibuni ya kuwateka, kuwaua na kupora pikipiki za Waendesha bodaboda mjini Kahama.

MAPANDE ameongeza kuwa zoezi hilo lililoanza Juni 10 na kukamilika Juni 30 mwaka huu ni endelevu ambapo pikipiki zinazokamatwa na usajili wake kutiliwa mashaka zinakabidhiwa kwa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi ili kubaini kama pikipiki hizo zimeibwa kutoka maeneo mengine na kuletwa mjini humo.

Hivi karibuni mkuu wa wilaya ya KAHAMA FADHILI NKURLU aliwataka boda boda kushirikiana na vyombo vya ulinzi kuimarisha ulinzi miongoni mwao akiwaasa kuwa makini na kufuata na kuhakikisha kila bodaboda inakuwa na kituo maalum kinachotambulika.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata