BASHE:TUMEFANYA MAKOSA TUANZE UPYA TUSONGE.

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe
Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe amefunguka na kusema kwa miaka mingi wabunge wamekuwa wakilalamika juu ya mikataba mibovu ya madini na kusema hata wananchi ambao madini hayo yapo katika majimbo yao hawajanufaika nayo kwa lolote lile.

Hussein Bashe anakiri wazi kuwa ni kweli makosa yamefanyika lakini anamshukuru Rais Magufuli kwa kuweka nia ya kutaka kushughulika na mambo hayo huku akisema siyo vibaya kama taifa kuanza upya.

"Kwa miaka mingi watu ambao tunatoka maeneo yaliyokuwa na migodi mikubwa tumekuwa tikilalamika sana juu ya marejesho na uwepo wa uwekezaji wa migodi hiyo, mimi natoka Nzega ukiniuliza leo 'Golden pride' ya Nzega toka imeanza miaka ya tisini mpaka imeondoka imefunga mgodi tumepata nini wananchi wa Nzega jibu hakuna na bahati mbaya ni kwamba kwa muda mrefu taifa lote limekuwa likilalamika, hata kipindi mimi nipo nje ya Bunge wabunge walikuwa wanalalamika wakisema juu ya mikataba, juu ya sheria kwamba hatufaidiki" alisema Bashe
Mbunge huyo aliendelea kutoa sifa zake kwa Rais John Pombe Magufuli na kueleza kuwa hili jambo lisiishie tu kwenye sheria bali hata mikataba ya madini inapaswa kupitiwa yote.

"Kwa hiyo katika kipindi chote hicho nani alikuwa wa kuthubutu? Binafsi nampongeza sana Rais Magufuli kwa maamuzi ya kuamua kufukua hili dude, si vibaya kama Taifa kuanza upya, kwani taifa hili mwaka 1961 lilianza upya hakuna tatizo tumefanya makosa huko nyuma leo tuanze upya, na mimi hili suala la Rais kusema yupo tayari kukaa nao mezani kutaka na bunge lipitie sheria tu lisiishie kwenye sheria tu bali liende mbali zaidi mpaka mikataba yote ipitiwe ya madini, tunaweza kupitia sheria leo tukafanya mabadiliko ya sheria lakini mikataba iliyopo isiathiriwe na sheria iliyopo sababu sheria haiwezi kurudi nyuma bali inaanzia pale ilipoanzia kwenda mbele" alisisitiza Hussein Bashe  

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata