BAADA YA KUTEKWA ROMA MKATORIKI ASEMA PUNDE ATALIAMSHA DUDE.

Rapa Roma Mkatoliki

Rapa Roma Mkatoliki ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu katika muziki baada ya kupata matatizo ya kutekwa amekiri wazi kuwa saizi yuko poa na tayari ameshajipanga kwa ajili ya kuliamsha dude muda wowote kutoka sasa.
Roma Mkatoliki amefunguka hayo jana baada ya kutembelea shule ya msingi Mchikichini iliyopo Mbagala na kutoa vitabu kwa wanafunzi wa darasa la saba pamoja na kuwapa hamasa juu ya kuweka juhudi katika masomo ya sayandi ikiwepo somo la hesabu.

Roma anasema anajua wazi baada ya matatizo yaliyomkuta kuwa watu wanashauku kubwa kutaka kusikia ngoma yake ya kwanza itakuaje, show yake ya kwanza itakuaje ila anadai kuwa atajibu maswali hayo ya mashabiki wake hao muda si mrefu baada ya kuliamsha dude.

"Mpango wa kuachia wimbo upo sababu nina muda mrefu nipo kimya na naona watu wana kiu kubwa kuona Roma anaachia wimbo upi na ataimba nini ndani yake, show yake ya kwanza itakuaje na atafanyia wapi, hayo nimekuwa nikiulizwa sana saizi tupo kwenye mfungo wa mwezi wa Ramadhan hivyo naona mawazo ya watu yameelekea huko na mimi najipa muda halafu baada ya hapo na mimi niliamshe dude, kwa sababu dude naliamsha kweli hivyo sitaweza kusema itakuwa ni tarehe gani ila muda wowote kinawaka" alisema Roma Mkatoliki.

Roma Mkatoliki mara ya mwisho ameachia wimbo wa kushirikiana na Moni Centrozone 'Usimsahau Mchizi' ilikuwa mwanzoni mwa mwezi wa kwanza kabla ya wasanii hao wote wawili kutekwa na watu wasiojulikana mwanzoni mwa mwezi wa nne mwaka huu.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata