AMWACHA MTOTO MGAHAWANI KISHA AENDA KUJINYONGA KWA KANGA.

Manyoni. Mtu mmoja amekutwa amejinyonga kwa kanga hadi kufa akiwa nyumbani kwake eneo la Mamatatu, kijiji cha  Muwanzi nje kidogo ya Hopitali ya Wilaya ya Manyoni.

Diwani wa kata hiyo, Maghembe Machibula amesema tukio hilo limetokea jana Jumatatu saa tatu asubuhi.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumanne, Machibula amesema kabla ya kujinyonga, marehemu alienda katika mgahawa wa Agnes Charles kwa ajili ya kunywa chai huku mgongoni akiwa amembeba mtoto wake mwenye umri wa miezi tisa, mgongoni.

“Kabla hajanywa chai alimuacha mtoto wake kwa mhudumu huyo kwa madai ya kwenda kujisaidia lakini hakurudi na baadaye ndipo ilipobainika kuwa alikwenda kujinyonga,” amesema Diwani huyo.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Jamil Mbwana amethibitisha kutokea tukio hilo ingawa alidai hana taarifa zaidi za marehemu kwa kuwa ni mhamiaji.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata