KAMPUNI YA BARRICK YAKUTANA NA RAIS MAGUFULI YAKUBALI KULIPA MADENI YOTE YANAYODAIWA KUPOTEA.


Kampuni ya Barrick Gold Corporation (mmiliki mkuu wa Kampuni ya ACACIA Mining Limited) imesema iko tayari kufanya mazungumzo na serikali ya Tanzania na kulipa pesa zote zinazodaiwa kupotea kwa kipindi chote ambacho imefanyakazi hapa inchini.

Hatua hiyo imefikiwa Ikulu Dar-es-Salam leo kwenye mazungumzo baina ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli na mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation Profesa John Thonton aliyekuja kufuatilia mgogoro wa kibiashara unaoendelea nchini.

Taarifa kutoka Ikulu iliyotolewa leo jijini Dar-es-salaam imesema Profesa Thornton amesafiri kwa ndege binafsi kutoka nchini Canada hadi Tanzania ili kuongelea suala la pesa zinazodaiwa kupotea kwenye biashara ya migodi inasimamiwa na ACACIA nchini.

Katika mazungumzo hayo Profesa Thornton amesema kampuni Kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.

Kataika mazungumzo hayo ambayo yamehudhuriwa pia na Balozi wa Canada nchini Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba  nchini Profesa Palamagamba Kabudi pande zote zimekubaliana kumaliza mgogoro huo wa mchanga wa dhahabu ulikuwa ukisafirishwa nje ya nchi.

Profofesa Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.

Rais Magufuli amesema Serikali inakaribisha mazungumzo hayo na itaunda jopo la wataalamu watakaojadiliana na Barrick Gold Corporation ili kufikia makubaliano ya kulipwa fedha zinazodaiwa na namna kampuni hiyo itakavyoendesha shughuli zake kwa maslahi ya pande zote mbili.

Katika hatua nyingine, pamoja na kukubali kulipa fedha zinazodaiwa na serikali ya Tanzania, Profesa Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu (smelter) hapa nchini.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amevionya vyombo vya habari vinavyowataja Marais wastaafu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete vikiwahusisha na taarifa za kamati mbili za uchunguzi wa Mchanga wa Madini (Makinika) kwamba viache mara moja.

Onyo hili amelitoa kwa sababu baada ya kupitia taarifa zote mbili hakuna mahali ambapo Mkapa na Kikwete wametajwa hivyo vyombo vya habari viache kabisa kuwachafua hawa wazee kwa kuwa wamefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa letu. 


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata