WANAFUNZI HEWA KAHAMA WASABABISHA HASARA YA SHILINGI MILIONI 225

Wanafunzi hewa waliopatikana Wilayani Kahama wameitia hasara serikali ya shilingi milioni 225 kuanzia Januari hadi Agosti mwaka huu baada ya kubainika katika shule za sekondari na msingi kuna wanafunzi hewa.

Hali hiyo imeelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu wakati akiongea na wakuu wa idara katika Halmashauri ya Mji wa Kahama ambapo amesema kamati yake maalumu aliyounda imebaini kuwepo kwa wanafunzi hewa elfu 29  katika shule za msingi

Serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakani imekuwa ikituma fedha kila shule kwenye mpango wake wa elimu bure lakini tayari baadhi ya maofisa elimu, waratibu Kata, Walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari wamebuni mbinu za kula fedha hizo kwa kuweka wanafunzi hewa kwenye shule zao

Kufuatia hali hiyo Mkuu huyo wa Wilaya ameunda kamati ya kuchukua takwimu sahihi katika Halmashauri zote tatu na kubaini takwimu za idadi za wanafunzi zilizotolewa hazikuwa sahihi ambapo kila baadhi ya shule imeonekana idadi ni kubwa kuliko hali halisi iliyopo.

Mkuu huyo wa Wilaya ametoa siku tatu kwa Halmashauri zote kuleta takwimu sahihi ambazo zitalingana na idadi yake aliyonayo ambayo imepatikana baada ya kuunda kamati hiyo iliyofanya uchunguzi Wilaya yote ya Kahama


Aidha Nkurlu ametoa onyo kali kwa wale watakaobainika kuhusika na wanafunzi hao hewa atawachukulia hatua kali bila kujali nyazifa zao na baada ya kuwachukulia hatua kali watalazimika kuzilejesha fedha hizo zilizoliwa kwa mgongo wa wanafunzi hewaSAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata