MWENYEKITI WA KIJIJI CHAMBO WILAYANI KAHAMA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA VIKONGWE WAWILI.

Jeshi la polisi Wilayani Kahama limemfikisha Mahakamani mwenyekiti wa kijiji cha Chambo Clement Shija kwa tuhuma za mauaji ya vikongwe wawili waliouawa na wananchi wenye hasira baada ya kutuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ushirikina vijijini hapo

Awali mwenyekiti huyo alikuwa ametoroka baada ya mauaji hayo hali iliyofanya polisi waendeshe msako uliofanikisha kumkamata kwa madai ya kuhusika katika mauaji hayo baada ya mtoto wake Jovita Clement kufariki katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama na yeye kudai amerongwa na vikongwe hao

Akisomewa mashitaka hayo ya mauaji katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama na mwendesha mashitaka Peter Masatu mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi Kenedy Mtembei imedaiwa mshitakiwa ametenda kosa hilo Agosti mwaka huu baada ya mtoto wake kufariki

Aidha mwendesha mashitaka huyo amedai mshitakiwa huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa kijiji hicho baada ya kufiwa na mtoto wake aliongoza mamia ya wanakijiji wenzake kufanya mauaji hayo kwa kuwaua vikongwe hao na kisha kuwachoma moto

Masatu amedai mtuhumiwa huyo amechangia kuuwawa kwa vikongwe hao ambao ni Masele Siyantemi umri miaka 60 na Minza Mzwazwa umri wa miaka 60 na baada ya mauaji hayo  mtuhumiwa alitoroka mpaka alipokamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani hapo

Hata hivyo mtuhumiwa hakutakiwa kujibu lolote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kisheria wa kusikiliza kesi za mauaji na Hakimu Mtembei ameahilisha kesi hiyo mpaka septemba 12 mwaka huu kesi hiyo itakaposikilizwa tena na  amerudishwa mahabusu katika gereza la Wilaya ya KahamaSAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata