MKAZI WA KAHAMA PROCHESE ULOMI AFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KUMLAWITI MTOTO WAKE.

Mahakama ya Wilaya ya Kahama jana  imemhukumu kifungo cha maisha jela Prochese Ulomi (35) mkazi wa Kakola wilayani Kahama baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa kike mwenye umri wa miaka (6).

Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Evodia Kiharuzi amesema Ulomi amepatikana na hatia hiyo baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri pasipo kuacha shaka.

Kiharuzi amesema Mtuhumiwa atatumikia kifungo cha maisha gerezani ili iwe fundisho kwa watu wengine kwenye jamii wenye tabia kama hiyo ambayo haipaswi kuingwa.

Awali mwendesha mashitaka wa polisi Shabani Zuberi amedai katika shauri hilo la jinai namba 307 la mwaka 2016 kuwa Olomi amekiuka kifunga namba 154 sura 16 ya kanuni ya adhabu kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Zuberi ameiambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo june 2 mwaka huu na kisha kukimbia  hadi alipokamatwa na kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Juni 5 mwaka huu ambapo alisomewa shitaka hilo na kukana.

Kabla ya hukumu mtuhumiwa alipopewa nafasi ya kujitetea ameiomba mahakama impunguzie adhabu kwani ni kosa lake la kwanza na ana familia inayomtegemea hali ambayo hakimu Kiharuzi alitupilia mbali maombi hayo na kumtupa jela kifungo cha Maisha.
SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata