KUPANDA KWA BEI YA USHURU KATIKA MACHINJIO YA BUSOKA KAHAMA KWAZUA UTATA .

Siku moja baada ya idara ya mifugo katika Halmashauri ya mji wa kahama kutangaza kupandisha ushuru wa mifugo katika machinjio ya busoka kutoka shilingi elfu moja na mia tano hadi kufikia shilingi elfu tano iliyopingwa na wafanyabiashara ya nyama tayari zoezi hilo limesimamishwa mpaka watakapokubaliana kwa pamoja

Zoezi la kusimamishwa kwa bei hiyo mpya limetangazwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo jana Abel Shija baada ya redio Free Afrika  kupitia kipindi chake cha matukio kutangaza mgomo wa wafanyabiashara kupinga kupanda kwa bei hiyo ya ushuru wa machinjio hayo

Mwenyekiti huyo amesema ameamua kusitisha kupanda kwa bei hiyo mpaka pale Halmashauri yake itakapokaa na wafanyabiashara hao na kukubaliana kwa pamoja juu ya kupandisha kwa ushuru huo kutokana na awali idara ya mifugo imepandisha bila kuwashirikisha

Hata hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa kahama Anderson Musumba ameonyesha kushitushwa na idara yake kupandisha bei hiyo bila ofisi yake ya utawala kuwa na taarifa na ushuru huo mpya ulikuwa uanze kulipwa September 1 mwaka huu wakati mwaka wa fedha huanza pamoja na bajeti mpya julai 1 kila mwaka

Kufuatia hali hiyo Mwenyekiti wa wafanyabiashara ya nyama mjini kahama Renatus Andrew ameipongeza Halmashauri hiyo kupitia Mwenyekiti wake Shija kwa uamuzi wake wa kusitisha kupanda kwa ushuru huo hali ambayo amedai ni usikivu wa kilio kwa wananchi wa kahama kwa kuwa ungesababisha kupanda kwa bei ya nyamaSAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata