KAMPUNI YA ZUKU KUTOA HUDUMA BURE KWA MIEZI 3 KWA WATEJA WAPYA.


Kampuni ya burudani ya Zuku inayomilikiwa na Wananchi Group imesema wateja wapya wa Zuku watanufaika kwa kupata huduma za habari, burudani bure kwa miezi 3 ikiwa ni hatua ya kampuni ya Zuku kuunga mkono upatikanaji wa habari nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofa hiyo Meneja Mkuu  wa Zuku TV Tanzania Bw. Omari Zuberi alisema Zuku imeona kuna umuhimu mkubwa kwa watanzania wote kupata habari na burudani hatua itakayosaidia shughuli mbalimbali za maendeleo na uchumi kwa taifa pia ni sehemu ya kampuni yetu kusaidia jamii katika nyanja ya mawasilino. 

Mpango huu utasaidia kwa asilimia kubwa watu wa mjini na vijijini ambao watajiunga na Zuku kupata ofa hiyo kuanzia leo.

 "Ofa hii ya miezi 3 bure kwa wateja wapya wa Zuku, ni ofa endelevu kuanzia mwezi huu wa tisa. Kuanzia leo, mteja yeyote ambaye atajiunga na Zuku atapata kifurushi cha Zuku Smart bure kwa miezi 3” alisema Bw. Zuberi.

Alisema  kifurushi cha Zuku Smart kimepewa kipaumbele vipindi mbali mbali vya, filamu, vipindi vya watoto, chaneli za hapa Tanzania na Afrika, na kina jumla ya  chaneli 36 za kiditali na chaneli 18 za redio.
 "Ofa hii ni mojawapo ya mikakati ya Zuku ya kutoa huduma bora kwa bei nafuu. Sasa hivi, kifurushi hiki cha Zuku Smart ni cha bei nafuu zaidi Tanzania na huduma zetu zinapatikana kote nchini” alisema Zuberi.

Baada ya ofa ya miezi 3, wateja wanapata fursa ya kuendelea kutumia kifurushi cha Zuku Smart au kuchagua kati ya vifurshi vya Zuku kama vile Zuku Smart Plus (chaneli 46) Tzs 13,000, Zuku Classic (chaneli 74) Tzs 18, 000 na Zuku Premium (chaneli 101) Tzs 25, 000.

Hapo awali Zuku TV iliwapa wateja fursa ya kuzawadiwa vitu mbalimbali. Wateja ambao walilipia kifurushi kwa miezi sita kwa pamoja, walizawadia mwezi moja bure.  Pia wateja waliojiunga na Zuku Smart na kulipia miezi 12, walizawadiwa miezi miwili bure.

Kifurushi cha Zuku Smart kilibuniwa baada ya wateja wa Zuku kutoa  maombi ya kupata huduma ya burudani bora kwa bei nafuu ambayo inakidhi mahitaji ya familia nzima. Miongoni ya chaneli zinazopatikana  Zuku Tv ni Zuku Entertainment, Zuku Movies Max, Zuku Movies Hatua; Zuku Novella, Zuku Kids, Zuku Life, Zuku Swahili Movies na Zuku Sports.

Huduma za buradani bora kwa familia za  Zuku TV inapatikana  nchini za Tanzania, Kenya, Zambia, Uganda na MalawiSAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata