KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YASHUSHA NEEMA KWA WAKULIMA WA MAZAO YA MAHINDI,MTAMA,ULEZI NA SHAYIRI NCHINI.

MKURUGENZI WA WA MAWASILIANO WA KAMPUNI YA SERENGETI JOHN WANYANCHA AKIFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI JIJI MWANZA.
 

MWANZA

Kampuni ya bia ya Serengeti Tanzania Imepanga kutumia malighafi ya mazao ya nafaka ya ndani ya nchi hadi kufikia asilimia 80 kwa mwaka huu kutoka asilimia 60 ya awali.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni hiyo John Wanyancha katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika kiwanda cha Serengeti Mwanza.

Wanyancha amesema kuwa kwa sasa kampuni ya Serengeti inatumia malighafi za ndani zinazofikia tani 10,000 sawa na asilimia 60 ya malighafi yote inayotumia kuzalisha bia za kampuni hiyo kwa mwaka.

Akitaja malighafi hizo Wanyancha amesema kuwa ni Mahindi,Mtama,Ulezi na shayiri ambayo wanazipata kutoka kwa wakulima kupitia mradi wa Kilimo Biashara baada ya kampuni ya Serengeti kuwapatia mbegu bora ikiwa ni pamoja na kuwapeleka wataalamu wa kilimo katika maeneo yao.

WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA MWANZA WAKIWA KATIKA KIWANDA CHA BIA CHA SERENGETI MKOANI MWANZA.

Ameongeza kuwa mradi wa Kilimo Biashara wenye lengo la kutumia malighafi zinazozalishwa nchini ulionza miaka mitatu iliyopita umesaidia kutengeneza bia za kampuni hiyo kwa kutumia asilima 100 ya malighafi hizo.

Akizitaja aina za bia zinazotengenezwa na malighafi za hapa nchini kuwa ni pamoja na Pilsner, Kibo Gold, Kick, Uhuru na Senator Lager na kwamba bia mbili za Pilsner na Kibo Gold zimeshinda tuzo za kimataifa mwaka huu ikiwa ni kielelezo cha ubora wa hali ya juu wa bidhaa hizo.

Katika kufanikisha mradi wa Kilimo Biashara kampuni ya Bia ya Serengeti  inatoa mbegu zilizo na ubora  kwa wakulima bure, kuwaunganisha na taasisi za kifedha  ili kupata mitaji  inayohitajika  kwa ajili ya kilimo  cha mashamba makubwa  hali kadhalika  kuwaunganisha na wasambazi wa mbolea na dhana nyninginezo za kilimo.

 Mradi wa Kilimo Biashara kutoka kampuni ya Serengeti Hadi sasa   umeshawanufaisha  wakulima zaidi ya 100 kutoka mikoa ya Arusha, Manyara, Mbeya, Kilimanjaro, Singida, Morogoro, Shinyanga na  Dododoma ambao kwa pamoja wanalima takribani ekari 20,000 za mazao hayo.

 MENEJA WA UPISHI WA BIA YA SERENGETI ROLINDA SAMSON (KATIKATI) AKIWAELEZA WAANDISHI WA HABARI NAMNA YA UPISHI WA BIA UNAVYOFANYIKA KATIKA KIWANDA HICHO.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata