HUU HAPA UKWELI KUHUSU WAANDISHI WA HABARI 7 SHINYANGA WALIOKAMATWA NA POLISI.

Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mkoani shinyanga leo mchana walikamatwa na polisi wa kituo kidogo cha Bugarama wilayani kahama na kushikiliwa kwa muda baada ya safari yao kuhusishwa na maandamano ya ungana kupinga udikteta Tanzania UKUTA ambayo hata hivyo chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA leo kimeahirisha mpaka October moja mwaka huu

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Jumanne Muliro amethibitisha kukamatwa kwa waandishi hao kwa madai walikamatwa na baada ya mahojiano waliachiwa huru kuendelea na shughuli zao ingawa alisema walipata taarifa ya kundi la watu wanaojifanya waandishi wa habari kupita barabara hiyo.

Katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa shinyanga Steven Wang’anyi amesema waandishi hao akiwemo na yeye mwenyewe wamekamatwa baada ya kufika usawa wa kituo hicho cha bugarama walikuta kizuizi na kundi kubwa la askari wakiwa wamevaa kofia ngumu ambao waliamuru waandishi wote washuke pamoja na abiria wengine ambao baadae waliachiwa.

Wang’anyi amewataja waandishi waliokamatwa ni pamoja na Shija Felician toka kampuni ya Mwananchi mkoa wa Shinyanga Raymond Mihayo toka gazeti la habari leo Paulo Kayanda toka gazeti la Mtanzania Neema Sawaka toka gazeti la Nipashe Grayson Kakuru toka Televisheni ya TBC Frank Mshana toka Televisheni ya ITV pamoja na
yeye mwenyewe Wang’anyi toka Azam Tv  
Hata hivyo baada ya mahojiano waandishi hao walibainika walikuwa wakielekea kakola kwenye makabidhiano ya kituo cha Afya cha kata ya Bulyanhulu kilichojengwa na Mgodi wa Bulyanhulu ambacho kilikuwa kikikabidhiwa Halmashauri ya msalala na Askari mmoja mwenye cheo cha Sajenti alipiga simu katika mgodi huo kudhibitisha safari ya waandishi hao kwenda kakola

Pamoja na polisi kuwakamata waandishi hao baadhi yao waliwaeleza waandishi hao bila kutaja majina yao kuwa walipokea simu kutoka kwa viongozi wao mjini kahama juu ya safari ya waandishi hao kwenda kakola kwa kuhisi huenda walikuwa wakienda kushiriki maandamano ya UKUTA taarifa ambazo hawakuzifanyia kazi kwa makini na badala yake wakachukua jukumu la kuwakamata waandishi hao kwa dakika 32 na baadaye kuwaachia huru
SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata