CHAMA CHA WALIMU CWT KAHAMA CHAPINGA WALIMU WAKE KUKATWA MISHAHARA ILI KUSHONA SARE ZA MWENGE.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA WALIMU WILAYA YA KAHAMA VICTOR TANDISE.

KAHAMA
Chama cha walimu Tanzania wilayani Kahama kimepinga uamuzi wa halmashauri ya mji wa Kahama wa kuwakata mshahara wao kwa ajili ya kuchangia sare za mwenge wa Uhuru
kwa madai uamuzi huo haujawashirikisha walimu hivyo hawako tayari kukatwa mshahara wao

Akiongea na Kijukuu Blog mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Kahama yenye halmashauri mbili za mji na msalala  Victor Tandise amesema walimu wake wamepokea kwa masikitiko uamuzi huo wa kuwakata walimu shilingi elfu thelathini kwenye mshahara wao kinyume  na utaratibu wa utumishi wa umma

Tandise amesema mshahara ni haki ya mtumishi wa umma hivyo haupaswi kuingiliwa na mamlaka yoyote hivyo kama ni mchango wa kuchangia sare za mwenge wanapaswa kuchanga wenyewe bila kukatwa mshahara wa

Mmoja wa wakurugenzi katika halmshauri hizo Deogratias Kapami kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa kahama amesema wao walichofanya ni kurahisisha upatikanaji wa sare hizo kwa walimu ambao hawatokuwa na fedha taslimu za kulipia sare hizo kwa kuwakopesha na kisha kuwakata kwenye mshahara.
MFANO WA SARE ZA MWENGE WA UHURU ZILIZOVALIWA NA WATUMISHI WA BUKOBA MWAKA 2014

Hata hivyo Kapami amesema utaratibu wa kuwakata mshahara walimu hao ni wale ambao watasaini kwenye daftari la kukopa sare hizo huku akisisitiza swala la kushirikli mkesha wa mwenge ni la lazima kwa watumishi wa umma na kuvaa sare ni lazima


Pamoja na chama cha walimu wilaya kupinga hatua hiyo ya kukatwa kwa lazima ununuzi wa sare hizo Kapami amesema mtumishi  yoyote  ambaye atashiriki mkesha huo bila kuvaa sare na yule ambaye hata shiriki kabisa atachukuliwa hatua na yule ambaye hatakubaliana na kukatwa mshahara akanunue yeye mwenyewe kwenye duka atakaloona

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata