WANANCHI USHETU-KAHAMA WAMKUMBUKA LEMBELI BAADA YA MBUNGE WA SASA KUCHANGIA LAKI MOJA KWENYE HARAMBEE ILIYOHITAJI MILIONI 5.


Baadhi ya waumini wa Parokia ya Ifunde kata ya Sabasabini wamemkumbuka Mbunge wa zamani James Lembeli aliyekuwa akiwasaidia katika michango mbalimbali ya kanisa na vikundi katika jimbo hilo baada Mbunge aliyoko sasa Elias Kwandikwa kutoa mchango wa shillingi laki moja katika harambe ya kuchangia upanuzi wa kanisa hilo.

Sintofahamu hiyo imeibuka baada ya waumuni wa parokia hiyo kumualika Mbunge wa jimbo hilo kuwa mgeni rasmi kwa ajili ya kuchangia kiasi cha shillingi Millioni 5 kwa ajiri ya upanuzi wa kanisa la parokia hilo huku wakitegemea kuwa kiongozi huyo angetoa mchango mkubwa kuliko waumiumini wengine kama alivyokuwa akitoa Lembeli.

Waandishi wa habari walipenyezewa habari hii  na baadhi ya waumini walioshiriki na kukerwa na mchango wa Mbunge huyo ambao walisema kuwa ulikuwa hauna tija kwao na nibora angeahidi kutoa vifaa vya ujenzi kuliko kutoa kiasi hicho kidogo cha fedha ambacho hakiendani na hadhi aliyonayo ya uongozi.

“Mimi mwenyewe kama muumini wa kanisa hili nimetoa kiasi cha shillingi laki moja na arobaini na sita kiasi ambacho nimemzidi hata mimi na bado kuna wengine wametoa kiasi cha shillingi elfu hamsini kwa kila mtu na hivyo kupatikana kiasi cha shillingi Million 3.1 ambayo laki moja ni mchango wa Mbunge” kilisema chanzo hicho cha habari.
ALIYEKUWA MBUNGE WA JIMBO LA KAHAMA JAMES LEMBELI.

Kilisema kuwa kiwango hicho cha shillingi Millioni 5 kilichokuwa kikitegemewa kuchangishwa katika harambe hiyo tuliamua kumwalika mbunge kama mgeni rasmi tukiwa na matumaini kuwa angetuchangia hata nusu ya kiwango hicho lakini hali ilikuwa tofauti na tulivyokuwa tunategemea.

Waaumini hao wameongeza kuwa   baada ya tamko la mgeni rasmi kutamka kuwa anatoa kiasi hicho waumini wote waliguna na kubaki wakinongonezana na kwamba amekosea labda ni Millioni moja lakin hali ilikuwa hivyo hivyo na kuwafanya wananchi kumkumbuka aliyekuwa Mbunge la Kahama Mjini James Lembeli aliyekuwa akishiriki vyema katika michango hiyo.

Ili kupata ukweli wa swala hili alipopigiwa simu Mbunge wa Jimbo la Ushetu ambae alikuwa mgeni rasmi katika harambe hiyo Elias Kwandikwa simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno alijibu hawezi kuongea yupo kwenye kikao.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata