WAFANYIKAZI WA SERIKALI WANAOFANYA SAFARI ZA KIHOLELA KUFUTWA KAZI UGANDA •

Waziri wa fedha nchini Uganda Matia Kasaija amesema kuwa maafisa huenda wakafutwa kazi iwapo watapatikana wamefanya safari zisizo na maana kwa kutumia fedha za serikali.
Tangazo hilo ni miongoni mwa hatua za kubana matumizi ya fedha za serikali ili kusaidia kufadhili miradi mingine
Bungeni,Bw Kasaija aliangazia kuhusu bajeti kubwa ya serikali inayogharimu dola bilioni 8 katika kipindi cha fedha cha mwaka ujao.
Anataka kuimarisha matumizi kuhusu ujenzi wa miundombinu na kuwekeza katika kilimo,utalii,biashara na teknolojia.
Lakini amesema kwamba hakutakuwa na kodi mpya na hivyobasi kuibua maswali vipi taifa hilo litaweza kujimudu.
Njia mojawapo ni serikali kuongeza kukopa.Bajeti hiyo inakasoro ya takriban dola bilioni 4.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata