TUMBILI ASABABISHA UMEME KUKATIKA NCHI NZIMA KENYA.

Kampuni inayozalisha umeme nchini Kenya ya KenGen yafahamisha kuwa kiza kilichotanda siku ya Jumanne nchini kwa ajili ya ukosefu wa umeme kilisababishwa na Tumbili.
Kwa mujibu wa kampuni hiyo ya kuzalisha umeme,nyani huyo alipanda katika paa la kituo cha umeme cha Gitaru na kuanguka kwa 'Transformer' na kuiharibu.
Hiyo ilipelekea kuharibika kwa mashine za kituo hicho cha umeme na kusababisha hasara ya zaidi ya 180MW .
Licha ya kuwa kituo hicho kimelindwa kwa uzio wa umeme ili kufukuza wanyama pori kampuni ilishindwa kutoa maelezo jinsi Tumbili huyo aliingia katika eneo hilo.
Maeneo mengi ya Kenya siku ya Jumanne yalikuwa giza baada ya kituo hicho kikubwa cha umeme nchini kupatwa na hitilafu za kimitambo zilizosababishwa na Tumbili.
Hata hivyo Tumbili huyo ameripotiwa kutolewa akiwa salama .SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata