JAMAA AMKA AJIKUTA AKIWA NA NYOKA MKUBWA KITANDANI.

Nyoka mkubwa ambaye alikuwa akiishi katika dari ya nyumba moja nchini Australia kwa takriban miaka 10 sasa ameamua kuingia katika chumba cha kulala.
Mwenye nyumba hiyo Trina Hibberd kutoka eneo la Queenland aliamka siku ya jumatatu na kumuona nyoka huyo mwenye urefu wa mita 5.2 amejipinda katika kitanda chake.
Aliwasha taa ya chumba hicho kabla ya mtaalam wa kushika nyoka Dave Goodwin kuwasli.

Bw Goodwin aliidunga sindano ya kulala nyoka hiyo yenye kilo 40 kabla ya kuiweka katika mkono wake na kuondoka nayo.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata