GAMBIA YAPIGA MARUFUKU MZIKI WA DANSI WAKATI WA MWEZI HUU WA MFUNGO WA RAMADHANI.

Serikali ya Gambia imetangaza marufuku ya kupiga muziki na kucheza densi kwenyemigahawa ya burudani katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Idara ya polisi nchini humo pia imetoa onyo kali kwa wananchi kutokiuka sheria hiyo iliyozuia muziki na densi mchana na usiku kwa kipindi cha mwezi mzima.
Mkuu wa polisi pia amewataka wananchi kuweka ushirikiano katika suala hilo na kuripoti kesi yoyote ya ukiukaji wa sheria hiyo.
Mnamo mwezi Desemba mwaka 2015, rais Yahya Jammeh alitangaza rasmi Gambia kuwa taifa la Kiislamu.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata