ZAIDI YA WATU 800 HALMASHAURI YA MSALALA WILAYANI KAHAMA WANG'OLEWA MENO BAADA YA KUBAINIKA YAMEOZA.

Zaidi ya watu 800 wakazi wa Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, wameng’olewa meno yao baada ya kubainika yameoza, ambayo yamesababishwa na utunzaji hafifu wa kinywa kwa wananchi ambao wengi wao wanaishi bila kupiga Mswaki.

Hali hiyo imebainishwa na Dk. Helen Young, kutokana nchini Uingereza ambaye ameongoza jopo la Madaktari 12 kutoka nchi hiyo, ambao wamekuja Tanzania, kutoa Elimu ya usafi wa Vinywa kwa Matabibu katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama.

Hata hivyo Young amesema, lengo lao  ilikuwa ni kutoa Elimu hiyo ambayo pia wameitumia kwa kuwataka wananchi wenye meno mabovu wafike kwenye vituo vilivyopangwa vya Lunguya na Bugarama, kupata Elimu hiyo ya Usafi wa Vinywa.

Katika zoezi hilo, jumla ya Matabibu 6 katika Halmashauri ya Msalala wamepatiwa mafunzo ya huduma ya Kinywa na wakati wa mafunzo hayo, idadi kubwa ya wananchi wamefika kupewa Elimu hiyo wamebainika meno yao yameoza.


Naye Mratibu wa mpango wa Huduma ya meno na Vinywa kutoka shirika la Bridge 2 Aid kutoka jijini Mwanza, Inno Bikele ambaye kwa kushirikiana na mgodi wa Bulyanhulu wametoa Huduma hiyo amesema, mpaka sasa wana watu zaidi ya 800 waliopewa huduma ya kung’olewa meno.


Bikele amesema, mwitikio wa wananchi kufika kupatiwa huduma hiyo ni mkubwa mno bila kujali umri wote wakiwa na tatizo la meno kuoza huku wengine wakiwa na umri mdogo na lengo lao ilikuwa ni kutoa Elimu lakini wamelazimika kutibu kwa kuyang’oa meno hayo.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata