MKUU WA MKOA WA ARUSHA ATAPELIWA SHILINGI MILIONI 10 KWA NJIA YA MTANDAO.

Mkuu wa Wilaya Arusha Fadhili Nkulu ameibiwa kiasi cha Tsh. milioni 10 na wezi wa mtandao ambao waliteka mawasiliano yake ya simu zake za mkononi kwa muda wa saa tatu na kutumia namba hizo kuomba fedha kwa watu wa karibu wa kiongozi huyo.

Akizungumzia sakata hilo jana ofisini kwake Arusha, Nkulu amesema kuwa jana majira ya saa kumi alasiri simu zake zilikuwa hazipatikani hewani mpaka saa tatu usiku ndipo aliposhtuka na kuanza kufuatilia na kugundua kuwa mawasiliano yake yalitekwa kwa muda.

Mkuu huyo amelaani vitendo vya wizi wa mtandao vinavyofanywa na watu wenye nia ovu, huku akiwataka Wananchi na wamiliki wa makampuni ya simu kuwa makini juu ya wizi huo wa mtandao ambao umeshamiri miaka ya hivi karibuni.

Mchezo mzima ni pale Msaidizi wa mkuu wa mkoa Yoitham Ndembeka ambaye alitumiwa ujumbe wa kumtaka atume fedha kupitia namba ya mkuu huyo wa wilaya...akielezea sakata hilo Ndembeka amesema kuwa baada ya kusumbuliwa na matapeli hao kwa muda ambao hawakutaka kupokea simu aliamua kuachana nao huku akitafuta namna ya kuonana ana kwa ana na Mkuu huyo wa Wilaya.

Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya simu ya Airtel kanda ya kaskazini alipotafutwa kujibu madai hayo simu yake haikupatikana hewani.

Wizi wa mtandao umeshamiri na kukua hasa katika kipindi hiki cha teknolojia za kisasa, hivyo Makampuni ya simu, Mamlaka husika za mawasiliano (TCRA) na wengineo sambamba na jeshi la polisi wanapaswa kuchukua hatua kupambana na uhalifu huo. 

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata