MBUNGE WA BUNDA MJINI, ESTER BULAYA(CHADEMA) AKAMATWA NA POLISI USIKU WA KUAMKIA LEO AKIWA HOTELINI JIJINI MWANZA

Mbunge wa jimbo la Bunda,Ester Bulaya amekamatwa na Jeshi la Polisi  jijini Mwanza.

Inaelezwa kuwa Polisi walivamia Hoteli aliyofikia mbunge huyo na kumkamata majira ya saa 7 usiku na kisha  kumpeleka  kituo cha kati cha Jijini Mwanza akiwa ameambatana na Mhe. Halima Mdee (Mb) , Joyce Sokombe (Mb) pamoja na Wakili John Malya. 

Taarifa za awali zinasema kuwa Mh Bulaya amekamata kufuatia agizo la Spika wa Bunge Job Ndugai la kutaka Mh Bulaya akamatwe na apelekwe jijini Dar es Salaam kwa kosa la kutohudhulia kwenye kamati ya Maadili ya Bunge 

Wabunge hawa pamoja  na  uongozi  wa  juu  wa  CHADEMA  Wako  jijini  Mwanza  kwa  ajili  ya  kikao  cha Baraza  Kuu  la  chama  hicho kinachofanyika leo katika Hotel ya Gold CrestSAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata