MOX PRODUCER WA TIVOL STUDIO MWENYE MCHANGO MKUBWA KATIKA KUKUZA NYIMBO ZA UTAMADUNI NCHINI TANZANIA.

DENNAMOCXY  AKIWA KATIKA STUDIO ZA TIVOL STUDIO JIJINI MWANZA.

EXCLUSIVE

Jumatatu ya leo nimepata fursa ya kumtembelea Producer maarufu wa nyimbo za Asili  nchini Mr.Mox ambaye anapiga mzigo katika studio maarufu ya nyimbo za Asili Tivol Studio zilizopo Nyasaka jijini Mwanza.

Jamaa amezaliwa Nchini Kenya miaka 30 iliyopita,Alipata Elimu ya msingi katika shule ya Mumius Boys, mwaka 1997 then akajiunga na sekondari ya Kakamega High School nchini Kenya kisha akajiunga na chuo cha IRGETON UNIVERSTY ambapo alikuwa akisomea Music na Information Technology(IT) kwa miaka miwili.

Baada ya hapo akanza rasmi mambo ya muziki mwaka 2007 ambapo alikuwa na studio yake iliyojulikana kwa jina la  G-HOOD ENTERTAINMENT nchni Kenya.

Kisha akaelekea Uganga kufanya kazi na UGZ RECORD kabla ya kurudi kenya na kumiliki tena studio yake iliyoitwa K RECODS ambayo ilikuwa hapo Kenya.

Katika kazi zake amewahi fanya Kazi za Bongo Fleva,Gospel,Utamaduni,Anasema katika kazi zake hakuna kazi ya mkono wake aliokubali kama nyimbo ya Mr Ong'eng'o wa Kenya na wimbo wa Saida Kaloli unaoitwa PESA INAWASHA. 
  
PRODUCER MOX AKIONYESHA UWEZO WAKE WA KUSUKA BEAT

Mwaka 2010 alifanya mawasilino na Mtangazaji wa Radio Star anaitwa Robby na ndiye alimuunganisha na Mkurugenzi wa Tivol Studio Mr.Madaraka Mchunguzi.

Anasema tatizo kubwa linamsumbua kwa sasa ni Lugha kati yake na wasanii wa nyimbo za asili ambao wengi wao hawajui kiswahili kabisa.

  
MOX KATIKA POZI
Kama wewe ni mpenzi wa nyimbo za Asili huyu ndiye Producer aliyetengeneza nyimbo zote za
.Bhudagala
.Saida Kaloli.
.Atomi Sifa
.Mchele mchele
.Bk sande wa Sekido
.Shemela
.Madebe
.Mwalimu George.
.Majita Jazz.
Wasumbwa Family
.Ya leo kali.
.Chime
.Hafsa Kazinja
Na wengine kibaoooooo

Usikose kumsikiliza katika Kipindi cha Asili yetu cha Radio Kahama Fm jumamosi hii kuanzia saa 1:00 asubuhi.,Ili uyajue mengi kuhusu yeye na uwepo wake wa Miaka Minne katika studio ya Tivol na harakati za kukuza Mziki wa Asili hapa Tanzania.

CONDENSER MIC AMABYO INACHUJA SAUTI NDANIYA TIVOL STUDIO.

  
HAPA NIKIGONGA NAYE INTERVIEW KATIKA STUDIO ZA TIVOL STUDIO

 
TIVOL STUDIO YA JIJINI MWANZA
 
WASANII KUTOKA RUKWA WAKISUBIRI KUFANYA KAZI KATIKA STUDIO ZA TIVOL STUDIO.
MR MOX AKIWA NA BAZIL FELEMONI AMBAYE NI MWANAFUNZI WA MOX PIA YUPO UPANDE WA PRINTING YA MAKASHA KATIKA STUDIO ZA TIVOL.

MOX AKIWA NA MSANII WA NELLEMBASANDO GRUOP TOKA RUKWA.

HAYA NDIYO MAWASILIANO YA MKURUGENZI WA TIVOL STUDIO MR.MADARAKA
SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata